Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameeleza kuwa, Ofisi yake itaendelea kuratibu Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ili kuendelea kuleta tija kwenye sekta hiyo.

Ameyasema hayo alipokutana na timu ya wataalamu kwa lengo la kujadili Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) tarehe 13 Machi, 2024 katika ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilijumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, Wasimamizi wa Programu ya ASDP II, Wataalam kutoka AGRA pamoja na Taasisi ya Axum Tanzania.

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa adhima ya Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Kilimo inaendelea kupewa kipaumbele ili kuinua uchumi wa Taifa na kujiletea maendeleo.