Padri auawa kwa kupigwa risasi

Watu wasiofahamika wakiwa na silala wamemuua kwa kumpiga risasi padri Padri Isaac Achi wa Kanisa la Katoliki nchini Nigeria.

Kasisi huyo ameuawa katika parokia yake kaskazini mwa Nigeria, kisha kuchoma moto kanisa katika kijiji cha Kafin Koro .

Mwili wa Padri Achi ulipatikana katika magofu yaliyoteketea ya jengo hilo.

Pia padri mwingine Collins Omeh, alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kuepuka moto huo na kupelekwa hospitalini.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa Padri Achi aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao wenye silaha, ambao alisema walikuwa wakipiga kelele za kijihadi.

Polisi wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa hao na taarifa zaidi kuhusiana la tukio hilo zitatolewa.