Latest Posts
Kivumbi Ligi Kuu Bara chaanza
Michuano ya Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, inaanza kutimua vumbi kwenye viwanja saba tofauti, Jumamosi wiki hii. Agosti 31, mwaka huu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitoa ratiba inayoonesha kuwa bingwa wa ligi hiyo atapatikana Mei 18, mwakani, wakati timu zote 14 zinazoshiriki zitakapokuwa uwanjani kuhitimisha mechi zake 26 kila moja.
Mramba: Kuleni nyasi
“Tupo tayari kula hata nyasi, lakini lazima ndege ya Rais inunuliwe”
Haya ni maneno aliyoyatoa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Pesambili Mramba wakati wa Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa Bunge lilipoelekea kukataa ununuzi wa ndege ya Rais.
Tujifunze kutokuwa wavivu wa kufikiri
Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE alisema, “Wengine humwona mwenzao anafanya kosa, badala ya kumwabia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri.
Nani anawashika mkono wajasiriamali?
Mwezi mmoja uliopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Barua ya biashara kwa BRELA”. Brela ni Mamlaka ya Uandikishaji Biashara na Leseni. Baada ya kuitoa gazetini niliituma pia barua hiyo huko Brela kwa njia ya barua pepe.
Tanzania siku si nyingi haitatawalika
Kwa siku za karibuni nchi yetu imegubikwa na mambo mengi ya kuudhi. Taifa linapokuwa na polisi wezi, waporaji na wauaji, usitarajie kwamba litaendelea kuwa salama. Taifa linapokuwa na majaji kama wale tulioambiwa na Mheshimiwa Tundu Lissu, hakika tumekwisha.
TAFAKURI YA HEKIMA
Polisi wangeweza kuepusha mauaji ya Mwangosi
Nianze kwa kutoa salamu za rambirambi na pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina.