JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Bukoba nani anasema ukweli?

Nchi hii kila kukicha inaacha maswali mengi. Mwanzo niliamua kunyamaza, lakini leo naona ni bora nihoji. Nahoji kutokana na taarifa zinazosambaa na kuzua mgogoro mkubwa ajabu katika mji wa Bukoba. Hapa inadaiwa kuna mapapa wawili – Mbunge Balozi Khamis Kagasheki na Meya Anatory Amani.

Wajasiriamali na mfupa wa huduma kwa wateja

Siku moja nilikuwa mjini Mafinga wilayani Mufindi katika Mkoa wa Iringa. Nikiwa hapo niliingia kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi nikiwa na lengo la kununua vifaa kadhaa vyenye thamani ya takribani shilingi laki tatu.

Ray C awalaani wauza ‘unga’

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amewalaani watu wanaofanya biashara ya kuuza dawa za kulevya nchini, akisema wanaharibu maisha ya vijana wengi.

Ponda naye anatafuta huruma ya waumini?

Mtakumbuka kuwa Agosti 10, mwaka huu, siku ya Idd Pili, iliisha vibaya kwa Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda. Siku hiyo katika simu yangu uliingia ujumbe mmoja kutoka kwa watu zaidi 25. Ujumbe huo ulisomeka hivi ‘Sheikh Issa

Ponda amepigwa risasi Morogoro, wataarifu waumini wengine kumuombea na kukemea mashambulizi ya silaha dhidi yake’.

Mtendaji mkuu Osha alalamikiwa Tughe

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, amelalamikiwa mbele ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), kuwa anawaongoza kimabavu wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Serikali.

Madudu ya mgodi wa Geita yaanikwa

Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kiasi cha Sh bilioni 38.2 tangu mwaka 2007 hadi 2013.