Latest Posts
Yah: Tuheshimu, tuthamini kazi tunazopewa
Mara nyingi huwa najaribu kufanya tathmini yangu ya kazi ambazo natakiwa kuzifanya kutokana na kuaminiwa na wenzangu, inaweza ikawa ushenga, ushereheshaji, kufanya utambulisho, kusoma hotuba au risala na kadhalika.
Inapotokea ukapewa heshima hiyo, unatakiwa kuheshimu kazi na kuwaheshimu waliokupatia kazi, unatakiwa kujali na kuthamini heshima hiyo kwa nafasi hiyo uliyopewa kwa imani ya waliokuteua.
Nakumbuka zamani ilikuwa tunafanya uchaguzi wa viongozi wetu kwa kuangalia hekima, busara na kujituma kwa mtu mwenyewe, vigezo vya shule havikuwa na maana sana kwa sababu hatukuamini kuwa shule peke yake ingeweza kukidhi haja ya busara, heshima na hekima.
Serikali izitendee haki shule zake
Kama tujuavyo nchini Tanzania kuna shule za aina mbili: Shule za Serikali (ambazo pia huitwa shule za umma) na shule za watu binafsi.
Katika Tanzania ya leo, shule za Serikali ni nyingi zaidi kuliko shule za watu binafsi. Hali haikuwa hivyo wakati wa ukoloni na katika miaka ya mwanzo ya Uhuru. Wakati huo shule za watu binafsi zilikuwa nyingi zaidi kuliko za Serikali.
Wafugaji Arusha, Simanjiro wajipanga
*Wanuia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Jamii ya wafugaji wa Kimaasai katika wilaya za Longido, Ngorongoro, Monduli (Arusha), na Simanjiro wanakabiliwa na wakati mgumu kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea.
Kwa miaka ya karibuni, hali ya tabianchi imekuwa mbaya. Kuna wakati mvua zinakosekana, na wakati mwingine zinanyesha kwa wingi. Miongoni mwa matatizo makubwa yanayotishia uhai wa mifugo na wafugaji wenyewe ni kupungua kwa majani yanayofaa kwa mifugo.
Tamisemi yatuhumiwa kuchakachua zabuni
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, anatuhumiwa kutoa zabuni ya uchapaji wa nyaraka za Serikali kwa Kampuni ya Yukos Enterprises Ltd ya mkoani Pwani bila kufuata taratibu.
Viongozi wa dini warejea na matumaini ya maendeleo
Viongozi 19 wa dini mbalimbali hapa nchini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wiki iliyopita wamerejea nchini kutoka katika ziara ya mafunzo nchini Thailand huku wakiwa wamefurahishwa na mafunzo waliyopata.
Mafunzo hayo yalitokana na jitihada za Serikali katika kuhakikisha elimu kuhusu masuala ya gesi asilia na mafuta inatolewa kwa wananchi wa kada mbalimbali, ili kufahamu mchakato mzima wa upatikanaji wa gesi asilia na mafuta.
Pia mafunzo hayo yalilenga kujua faida za gesi katika nyanja za kiuchumi na kijamii, changamoto zake na namna nchi nyingine zinavyotumia rasilimali hiyo katika kukuza uchumi.
Polisi Geita yafyata kwa watuhumiwa
Jeshi la Polisi mkoani Geita limeshindwa kuwakamata walinzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa hao — Maneno Nangi na John Magige — wamekwishaapa mbele ya mlalamikaji kwamba wako tayari kutumia fedha zao zote ili kuhakikisha kuwa wanajinasua kwenye tuhuma hizo.