JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Yah: Tusichezee lugha yetu, wengine wanajuta

Wakati tunatawaliwa, wakoloni wote kwa awamu zao yaani Wajerumani, Waingereza na hata Wareno na Waarabu, wakati wakipita kwa biashara zao sisi Wazaramo na Wandengereko tulikuwa tunawasiliana kwa shida sana. Kuna wakati tulikuwa tunatumia lugha ya alama kuwasiliana. Baada ya kuanza…

Fedha zako ni kipimo cha imani yako

Nianze kwa kuwasalimu wasomaji wetu. Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mchakato wa Katiba mpya, lakini ninasikitishwa na namna mwenendo wa Bunge hilo ulivyo.

Wiki iliyopita tumeshuhudia mgogoro wa kimakundi uliosababisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia vikao vya Bunge Maalum la Katiba.

Binafsi ninaamini kuwa pande zote zitakaa chini na kufikia mwafaka ili Taifa letu lipate Katiba mpya.

Sasa tuendelee na uchambuzi wa leo unaohusu uhusiano wa imani zetu na umilikaji fedha.

Tangu lini wapinzani wanawapenda wananchi?

Vyama vya upinzani vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika Bunge Maalum la Katiba vimesusia vikao vya bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu.

Wapinzani wametoa sababu zao za kuchukua hatua hiyo. Kwa mfano, wamesema Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, wametoa vitisho kwamba kukiwapo Serikali tatu Jeshi litachukua nchi.

NUKUU

Mwalimu Nyerere: Tudhibiti tofauti za maskini, matajiri “Tofauti kati ya watu maskini na watu matajiri zinaongezeka Tanzania. Inafaa tuwe macho. …lazima tuendelee kutumia Sheria za Nchi, na mipango mbalimbali ya Serikali, kuona kuwa tofauti hizi hazifikii kiasi cha kuhatarisha umoja…

Nani analinda bodaboda Dar?

Moja ya mambo yaliyomfurahisha Mkata Mitaa (MM) ni hatua iliyochukuliwa na Serikali kupiga marufuku pikipiki maarufu kwa jina la ‘bodaboda’, mikokoteni (makuta), baiskeli na bajaj kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

MM amefurahishwa na mpango huo kutokana na boda boda kuwa kero kwa waendesha magari na waenda kwa mguu wanaotumia barabara za katikati ya jiji.

Mwadui ni bora kuliko nyingine nchini – Julio

Kocha wa Timu  ya Soka  ya Mwadui ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ametamba kwamba timu hiyo itakuwa bora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuliko zote zinazoshiriki.

Akizungumza na JAMHURI hivi karibuni,  Julio amesema kuwa timu hiyo itatoa upinzani mkali kwa timu za Simba,  Yanga  na Azam FC.

“Simba na Yanga hakuna mpira pale bali kuna makelele, niliwahi kufundisha timu ya Kajumulo, sikuwahi kufungwa na Simba wala Yanga na hata sasa nikifanya usajili wangu hakuna timu ya kunifunga kati ya timu hizo,” amesema Julio na kuongeza: