Latest Posts
KAGAME NI MTIHANI Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa Uangalifu
Ni wazi kwamba nafasi inayoshikiliwa na Uganda na Rwanda katika roho ya uchumi wa Marekani na Uingereza ni kubwa kuliko nchi yoyote ile katika eneo la Maziwa Makuu kwa sasa.
Hakika Marekani na Uingereza wamelipa gharama kubwa kutengeneza miundo ya kiserikali, nguvu za kijeshi na saikolojia za kisiasa zinazoongoza nchi hizo miaka ya karibuni.
Watu walijiuliza maswali mengi kunako miaka ya tisini juu ya nguvu za Museveni na baadaye kasi ya RPF kuitwaa Rwanda, nchi ambayo ilikuwa imeanza kuimarika kama zilivyokuwa nchi nyingine barani Afrika. Hasa nchi ambazo zilikuwa zimeishi kwa amani toka uhuru mpaka miaka hiyo.
Mwanzoni mwa miaka ya tisini Rwanda ilikuwa na fedha yenye thamani kubwa. Ilikuwa pia na msaada mkubwa wa kijeshi kutoka Ufaransa. Raia wake walikuwa na kipato kizuri cha kutosha. Ilikuwa thabiti.
Matatizo yaliyokuwapo Rwanda miaka ya tisini yaliakisi matatizo yaliyokuwapo kwingineko barani Afrika kama vile vita za wenyewe kwa wenyewe, uongozi mbovu na uamuzi usiyo na tija, ufisadi wa wachache, upendeleo wa kikabila (Wahutu), undugu (nepotism) na zaidi suala la wakimbizi.
Wakimbizi wa Rwanda miaka ya ‘tisini mwanzoni’ walikuwa ni Watutsi waliokuwa wameikimbia nchi baada ya mapinduzi mwaka 1959 yaliyoiondoa dola ya mfalume Kigeri V muda mfupi kabla ya uhuru. Rwanda haikutofautiana na nchi nyingine nyingi barani Afrika.
Ukiilinganisha Rwanda ya sasa ya Kagame ambayo wapinzani wake wanaviziwa na kuuawa hata wakiwa nje ya nchi! Rwanda ambayo wakati wa uchaguzi raia wanapotea kimya kimya na baadhi kuokotwa wakiwa mizoga!
Hotuba ya Lissu iliyosababisha TBC1 ‘izimwe’
Aprili 12, mwaka huu, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu aliwasilisha maoni ya Wajumbe walio wachache katika Kamati Namba Nne kuhusu sura ya kwanza nay a sura ya sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati akiwasilisha, Televisheni ya Taifa (TBC1) ilikata matangazo yake katika kile kilichotafsiriwa na wengi kuwa ni kuuepusha umma kupata maoni ‘makali’ yaliyomo kwenye hotuba ya Lissu. Kwa kuzingatia haki ya wananchi ya kupata habari, JAMHURI inawaletea hotuba hiyo neno kwa neno. Endelea
UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’) ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa suala la muundo wa Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya Sita inahusu ‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya miaka thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya chama hicho imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi.”
Suala hili pia limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka mitatu iliyopita. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba wakati wa kuwasilisha Ripoti ya Tume yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar tarehe 30 Disemba, 2013: “Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu Rasimu ya awali ilipotolewa … ni Muungano wa Tanzania. Jambo kubwa limekuwa juu ya muundo wa Muungano.”
Umuhimu wa suala hili unathibitishwa pia na uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum kuelekeza kwamba Kamati zake Namba Moja hadi Kumi na Mbili zianze kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Haya ni maoni ya wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne juu ya Sura hizi mbili.
Kipande, Magesa wakoroga ICT bandari
Mamlaka ya Bandari Tanzania imegeuzwa sehemu ya ulaji wa hali ya juu. Hata hivyo, kutokana na mtandao mpana wa kuchota fedha unaoanzia wizarani hadi bandarini, yeyote anayetaka kuonesha paka yuko wapi, basi anaishia ama kufukuzwa kazi kwa njia ya vitisho, au kufanyiwa ‘kitu mbaya’.
Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, anamkingia kifua Mkurugenzi wa ICT, Phares Magesa, ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kuzamisha jahazi la bandari Tanzania.
Baada ya kuchapisha sehemu ya kwanza ya matukio yanayoendelea bandarini, wiki hii JAMHURI inakumegea sehemu tu kati ya madudu mengi yanayoendelea bandarini, ambayo kwa kila hali yanadhihirisha kuwa Mkurugenzi Mkuu, Madeni Kipande, ama hajui kitu kinachoitwa utawala wa sheria, au amedanganywa na watu wanaombeba pale Ikulu, hivyo amepoteza mwelekeo.
Ifuatayo ni sehemu ya barua ya ushauri wa kitaalamu, ambayo ilitolewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi, Mei mwaka jana, akieleza hatari inayoinyemelea bandari kutokana na mfumo wa mawasiliano (Information and Communication Technology – ICT) kuchezewa katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kupoteza mapato, imani ya wateja na kuhatarisha mizigo inayopitia bandarini.
Kwa mshango wa wengi, Dk. Jabir Bakari aliyeandika barua hii na kutoa ushauri, kwa mizengwe tu kama alivyosema Kipande kwenye kikao kati ya Wakurugenzi wa Bodi na Dk. Mwakyembe, Agosti mwaka jana huko Dodoma, kuwa “yeye ni mteule wa Rais na hivyo wakurugenzi hawambabaishi”, Kipande alifanya mbinu Dk. Jabir akafukuzwa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Bandari kwa kutoa ushauri huu. Ifuatayo ni tafsiri isiyo rasmi ya barua hiyo. Endelea…
Nyalandu aanza kuliliza Taifa
*Marekani yapiga marufuku nyara kutoka Tanzania Uamuzi tata na wa kijazba wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, umeanza kuleta athari kwa tasnia ya uwindaji wa kitalii nchini. Marekani imepiga marufuku nyara zinazotokana na ndovu kutoka Tanzania kuingizwa nchini…
Wakubwa wanavyotafuna Bandari
Majambazi wajitangazia Serikali
*Wajiundia Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo
*Wabuni bendera, mahakama na polisi yao
*Vijiji vyawatii, waendesha ujangili, ujambazi
Watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na majangili, wamejiundia serikali ndani ya Msitu wa Igombe mkoani Tabora, JAMHURI inathibitisha.
Wamejiundia uongozi madhubuti pamoja na jeshi walilolipa jina la Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa huenda idadi ya watu hao ikawa kubwa kuliko inavyodhaniwa, kwani wanadaiwa kusambaa ndani ya misitu minene katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Pia wapo katika maeneo kadhaa ya Mkoa wa Kigoma.
Imebainika kuwa watu hao wapo katika Msitu wa Igombe uliopo wilayani Uyui na kusambaa katika mapori mengine ya Malagarasi na Myowosi; na walianza kujiimarisha tangu mwaka 2010.
Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanaounda ‘serikali’ hiyo wanatoka katika makabila kadhaa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga, Arusha, Kigoma na katika mataifa jirani, hasa Burundi.
“Serikali” hiyo batili ina jeshi lake la ulinzi, jeshi la polisi, mahakama na vyombo vingine vya utawala.
Shughuli kuu zinazofanywa ni ujambazi, ujangili, kilimo cha bangi, biashara ya mbao, uuzaji bunduki pamoja na risasi; na uhalifu wa aina nyingine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, amezungumza na JAMHURI na kusema, “Ni kweli tuna tatizo hilo. Lipo na ni kubwa. Serikali imeshalitambua, na hatua zinachukuliwa.”
Mwasa, licha ya kukiri, hakutaka kuingia kwenye undani wa suala hilo katika kile kinachoonekana kuwa ni kutotaka kutibua hatua za kiusalama zilizopangwa kuchukuliwa na vyombo vya dola katika kukabiliana na genge hilo.
Hata hivyo, maneno ya Mwasa katika kuthibitisha ukubwa wa jambo hili ni haya, “Kweli tatizo lipo…ni kubwa kuliko unavyofikiri.”
Watu wawili waliokamatwa na baadaye kutoroka kutoka mikononi mwa kundi hilo wamesema genge hilo ni masalia ya wale walioshughulikiwa na Serikali mwaka 2010. Majina ya watu hao tunayahifadhi kutokana na sababu za usalama wao.
“Kuna jeshi lenye askari wa jadi wenye bunduki za SMG (Sub Machine Gun), na magobore. Wanaendesha uasi. Wamepandisha bendera ya bluu, imeandikwa Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo. Wahalifu wengi wageni wanatoka Burundi. Wanashirikiana na Wasonjo, Wasukuma na Waha.
“Shughuli zao ni kilimo cha bangi, kupasua misitu, uwindaji haramu na n.k. Wana watemi wao. Kila mtemi analindwa na askari wasiopungua 20,” anasema mmoja wa watoa habari wetu.
Uimara wa magenge hayo ya wahalifu yaliyojiimarisha yamewafanya hata wananchi na viongozi wa vijiji jirani na mapori wanamoishi, wawe watiifu kwao.
“Ukiwa na tatizo unaenda msituni kuomba msaada wa askari kukukamatia mhalifu au mbaya wako. Wanatumwa askari wanakuja kukuteka na kukupeleka huko msituni.
Habari mpya
- Kihongosi akagua utekelezaji miradi ya bil. 2.5 Nzega
- Tume ya uchunguzi yakutana na Katibu Mkuu Mnyepe, Gugu
- RPC Songwe aongoza kuuaga mwili wa Ex Sajenti Perpetua
- Kinywaji kipya chazinduliwa Dar
- Tanzania, Malawi wasaini mkataba kuimarisha biashara za wafanyabiashara wadogo
- Samba mbaroni kwa tuhuma za kukutwa mirungi Same
- Kamati ya ushauri Kibaha yapitisha bajeti ya bilioni 66.7/- kwa mwaka wa fedha 2026/2027
- Zelensky: Urusi inajiandaa kufanya mashambulizi Zaidi
- Asante TCRA, tusiruhusu vyombo vife
- Waziri Mkuu Mwigulu avutiwa kasi utekelezaji mradi wa EACOP, kuzalisha ajira, kukuza uchumi
- Naibu Waziri Dk Dugange atoa rai kwa watendaji kulipa umuhimu suala la uchumi wa buluu
- Mawaziri wakutana Lushoto kutafuta suluhu ya migogoro ya wananchi Tanga
- TMA yatoa tahadhari ya hali ya mbaya kwa siku tano
- Soma Gazeti la Jamhuri Februari 17 – 23, 2026
- Mkutano wa waandishi wa habari kuhusu ziara za kikazi alizofanya Rais Dkt. Samia