JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Mwigulu kata pua uunge wajihi

Juma lililopita nikiwa nafuatilia Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge, nilimshuhudia na kumsikia Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, akieleza matukio ya vifo vya raia katika maeneo kadhaa nchini, vilivyotokea kwenye shughuli za kisiasa na akahoji nafasi ya kisheria kuwashughulikia wahusika na waratibu wa matukio hayo badala ya wale wanaoshiriki katika maelezo yake.

Matakwa ya Rwanda yasiivunje EAC

 

Kwa muda wa mwezi mmoja sasa uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umezorota. Uhusiano huo umezorota baada ya matukio mawili. Tukio la kwanza ni ushauri  Rais Jakaya Kikwete aliompa Rais Paul Kagame wa kuzungumza na waasi wa kundi la FDLR kwa nia ya kurejesha amani. La pili ni Tanzania kupeleka majeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na waasi wa M23.

Hii ndiyo dawa ya kuepuka bomoabomoa

Katika miaka ya 1980, bendi moja ya muziki wa dansi hapa nchini ilitunga wimbo uliokuwa na kibwagizo cha “bomoa ee, bomoa ee, tutajenga kesho!”

Kocha wa Nigeria matatani

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limethibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa Shirikisho la mchezo huo nchini Malawi (FAM), kuhusu matamshi yaliyotolewa na Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi, yanayohusishwa na ubaguzi wa rangi.

Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (5)

Katika sehemu ya nne, Dk. Felician Kilahama alizungumzia kazi ya kutoa huduma bora za kijamii na kujenga miundombinu imara katika nchi yenye eneo kubwa. Alisema shughuli hiyo inahitaji ujasiri mkubwa na uzalendo wa hali ya juu. Sehemu hii ya tano na ya mwisho, Dk. Kilahama anatoa hitimisho.

Majaji wanaolinda wauza ‘unga’ wabainika

>>Gazeti hili sasa limeamua kuwataja kwa majina
>>Mahakimu nao wanawaachia mapapa kienyeji
>>Kigogo ofisi ya DPP, Mahakama Temeke, Kinondoni ni balaa

Mahakama kupitia baadhi ya majaji na mahakimu wasio waadilifu imebainika kuwa kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.Pamoja na Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP), nayo imelaumiwa kwa kufuta kesi katika mazingira ambayo hata mtu ambaye hakusoma sheria, anaweza kuyatilia shaka.

Wakati vyombo hivi vikikwamisha vita hii, lawama zimekuwa zikielekezwa kwa polisi na vyombo vingine vya usalama, ambavyo watendaji kazi wake wanafanya kazi usiku na mchana.