Latest Posts
Wakubwa wanavyotafuna Bandari
Majambazi wajitangazia Serikali
*Wajiundia Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo
*Wabuni bendera, mahakama na polisi yao
*Vijiji vyawatii, waendesha ujangili, ujambazi
Watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na majangili, wamejiundia serikali ndani ya Msitu wa Igombe mkoani Tabora, JAMHURI inathibitisha.
Wamejiundia uongozi madhubuti pamoja na jeshi walilolipa jina la Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa huenda idadi ya watu hao ikawa kubwa kuliko inavyodhaniwa, kwani wanadaiwa kusambaa ndani ya misitu minene katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Pia wapo katika maeneo kadhaa ya Mkoa wa Kigoma.
Imebainika kuwa watu hao wapo katika Msitu wa Igombe uliopo wilayani Uyui na kusambaa katika mapori mengine ya Malagarasi na Myowosi; na walianza kujiimarisha tangu mwaka 2010.
Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanaounda ‘serikali’ hiyo wanatoka katika makabila kadhaa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga, Arusha, Kigoma na katika mataifa jirani, hasa Burundi.
“Serikali” hiyo batili ina jeshi lake la ulinzi, jeshi la polisi, mahakama na vyombo vingine vya utawala.
Shughuli kuu zinazofanywa ni ujambazi, ujangili, kilimo cha bangi, biashara ya mbao, uuzaji bunduki pamoja na risasi; na uhalifu wa aina nyingine.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, amezungumza na JAMHURI na kusema, “Ni kweli tuna tatizo hilo. Lipo na ni kubwa. Serikali imeshalitambua, na hatua zinachukuliwa.”
Mwasa, licha ya kukiri, hakutaka kuingia kwenye undani wa suala hilo katika kile kinachoonekana kuwa ni kutotaka kutibua hatua za kiusalama zilizopangwa kuchukuliwa na vyombo vya dola katika kukabiliana na genge hilo.
Hata hivyo, maneno ya Mwasa katika kuthibitisha ukubwa wa jambo hili ni haya, “Kweli tatizo lipo…ni kubwa kuliko unavyofikiri.”
Watu wawili waliokamatwa na baadaye kutoroka kutoka mikononi mwa kundi hilo wamesema genge hilo ni masalia ya wale walioshughulikiwa na Serikali mwaka 2010. Majina ya watu hao tunayahifadhi kutokana na sababu za usalama wao.
“Kuna jeshi lenye askari wa jadi wenye bunduki za SMG (Sub Machine Gun), na magobore. Wanaendesha uasi. Wamepandisha bendera ya bluu, imeandikwa Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo. Wahalifu wengi wageni wanatoka Burundi. Wanashirikiana na Wasonjo, Wasukuma na Waha.
“Shughuli zao ni kilimo cha bangi, kupasua misitu, uwindaji haramu na n.k. Wana watemi wao. Kila mtemi analindwa na askari wasiopungua 20,” anasema mmoja wa watoa habari wetu.
Uimara wa magenge hayo ya wahalifu yaliyojiimarisha yamewafanya hata wananchi na viongozi wa vijiji jirani na mapori wanamoishi, wawe watiifu kwao.
“Ukiwa na tatizo unaenda msituni kuomba msaada wa askari kukukamatia mhalifu au mbaya wako. Wanatumwa askari wanakuja kukuteka na kukupeleka huko msituni.
Bandari Dar inakufa
*Mkurugenzi Mkuu Kipande aingiza ukabila, udini, majungu
*Wafanyakazi watatu bandarini wafariki kutokana na vitisho
*CCTV hazifanyi kazi tangu 2011, wachonga dola mil. 6.5
*Mnikulu Gurumo, Mtawa wampa kiburi, wachafua jina la JK
*Amdanganya Dk. Mwakyembe, amtukana Balozi wa Japan
Kuna kila dalili kuwa Bandari ya Dar es Salaam inakufa kutokana na uongozi mbovu uliojiingiza katika majungu, udini, ukabila na majivuno yasiyo na tija. Wafanyakazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamepoteza morali wa kufanya kazi kutokana na vitisho na matusi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Madeni Juma Kipande.
Hadi habari hii ya kiuchunguzi inachapishwa wafanayakazi watatu; Peter Gwamaka Kitangalala, Dotto Mbega na mwingine aliyefahamika kwa jina la Lyochi wamefariki dunia katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na shinikizo la damu lililozaa kiharusi baada ya vitisho vya Kipande.
Katika hali ya kuwavuruga wafanyakazi wa bandari, Katangalala alihamishiwa Mwanza na baada ya miezi miwili akahamishwa tena kwenda Lindi, huku akipewa vitisho kuwa muda wowote ajiandae kufukuzwa kazi. Kutokana na hofu, alipata kiharusi (stroke) akafa. Mbega kwa upande wake yeye alikuwa makao makuu Dar es Salaam, lakini kutokana na vitisho vya kila siku vya Kipande na wasaidizi wake, naye akapata kiharusi mwezi mmoja uliopita akafariki dunia.
Jumapili ya Machi 30, mfanyakazi mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Lyochi huku wengine wakisema ni Oluwochi mwenye asili ya Wajaruo, aliyehamishiwa bandari ya Kasanga, Sumbawanga naye aliaga dunia kwa ugonjwa huo huo wa kiharusi kutokana na mashinikizo ya Kipande.
“Uhalisia hali inatisha. Kipande anajinadi kuwa atamfukuza kila mtu, na kweli anafukuza anaajiri watu wa dini yake. Kuna kabila la Wahaya kutoka Kanda ya Ziwa, hilo utadhani waliwahi kushikana nalo ugoni. Mhaya yeyote aliyemkuta kazini ameapa kumg’oa. Amehamisha [Hassan M.] Kyomile kwa sababu ya kabila lake na kwamba aliomba kazi ya Ukurugenzi Mkuu,” kilisema chanzo chetu.
Kyomile amehamishwa Machi mwaka huu, kutoka makao makuu alikokuwa Mkurugenzi wa Ununuzi na kwenda kuwa Meneja wa Bandari Tanga.
Kikwete, Warioba wako sawa
Na Christopher Gamaina Wiki iliyopita nchi yetu, Tanzania, iliweka historia ya kipekee. Rais Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza alihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ikiwa ni siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini,…
Uchaguzi Chalinze ni huru, lakini si wa haki
Hivi karibuni nilishiriki mjadala unaohusu uamuzi wa Ridhiwani Kikwete kugombea ubunge Jimbo la Chalinze.
Kama ilivyo ada, mijadala ya aina hii mara zote imekuwa na mvuto. Kumekuwapo hoja kwamba wanaohoji uhalali wa mtoto wa Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge kupitia chama kinachoongozwa na babaake, ni wivu na husda!
Lakini wapo wanaoona kuwa kitendo hicho, ingawa ni haki yake ya kikatiba kama walivyo Watanzania wengine, hakiwezi kutolewa maelezo hata kikaweza kueleweka kwa wananchi walio wengi.
Sikukusudia kuendelea na mjadala huu kwa sababu tayari nilishaweka bayana faida na hasara za uamuzi wa Ridhiwani. Hata hivyo, makala kadhaa zilizoandikwa kwenye magazeti zimenifanya nirejee kutetea hoja yangu.
KAGAME NI MTIHANI
Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa uangalifu Je, ulipata kujua undani wa kisaikolojia na mazingira-mali vilivyosababisha dunia kuingia kwenye Vita Kuu ya Pili miaka ya 1939-1945? Kama unajua karibu tutafakari. Kama hujui naomba nikueleze kwa kifupi. “Sera ya huruma iliyofanywa…
- Serikali yakutana na Mjumbe Malaam wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola
- Samia azindua minara 758, maunganisho ya mkongo wa mawasiliano
- Rais Samia akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa minara 758 Dodoma
- Mwanamke ajichoma kisu tumboni baada ya kugombana na mpenzi wake
- Spika Zungu awahimiza wabunge kuachana na karatasi, wahamie mfumo wa kidigitali
Habari mpya
- Serikali yakutana na Mjumbe Malaam wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola
- Samia azindua minara 758, maunganisho ya mkongo wa mawasiliano
- Rais Samia akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa minara 758 Dodoma
- Mwanamke ajichoma kisu tumboni baada ya kugombana na mpenzi wake
- Spika Zungu awahimiza wabunge kuachana na karatasi, wahamie mfumo wa kidigitali
- Tanzania yaeleza mafanikio na fursa za uwekezaji sekta ya makazi katika kongamano la miji Africa
- Ofisi za Gazeti la Pambazuko zavunjwa na kuibwa nyaraka muhimu
- Watu 85 wakamatwa kwa uzushi wa kuibiwa nyeti, watatu waenda jela miezi sita
- Misaada ya maendeleo yapungua kwa asilimia 23.1 mwaka 2025
- Msajili vyama vya siasa ateta na Rais wa zamani wa Malawi Chakwera
- Doris Mollel umestahili tuzo ya WHO, umeokoa maisha ya wengi
- TBL yatoa wito wa hatua za pamoja za kukabiliana na hatari za pombe haramu Tanzania
- Jaji Masaju : Usuluhishi njia halali ya upatikanaji haki
- Mikopo ya Bilioni 2.6/- yatolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha
- CCM Kibaha Mjini yashirikiana na RITA kusogeza huduma kwa wananchi