Washtakiwa 40 akiwemo Lubea Manzi ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Master’ ‘ wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaa kwa makosa ya unyan’anyi kwa kutumia silaha mbalimbali.

Washtakiwa hao maarufu kwa jina la ‘Panya road wamefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi Oktoba 6, 2022 na kusomewa mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kuvunja nyumba usiku na kujeruhi watu maeneno mbalimbali ya Wilaya ya Ilala

Waendesha mashtaka mawakili wa Serikali, Michael Momboko, Magdalena Kisoka, Aziza Mhina mbele ya Mahakama walisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kati ya tarehe 19 – 21/09/ 2022 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala.

Momboko amesema kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kujeruhi wananchi kwa kutumia silaha za jadi kama nondo,mapanga, visu na kukimbia.

Watuhumiwa hao kwa pamoja walikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kutokana na mashataka wanayowakabiliwa nayo kutokuwa na dhamana.

Kesi hiyo inasikilizwa na Mahakimu watatu, Hakimu Mkazi Glory Nkwera, Fadhili Luvinga na Rehema Liana