Home Kitaifa PIGO: CHADEMA YAZIDI KUANGAMIA

PIGO: CHADEMA YAZIDI KUANGAMIA

by Jamhuri

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema CHADEMA inazidi kuangamia kutokana na kinachoendelea ndani ya chama hicho kuondokewa na viongozi pamoja na wanachama wake kutimkia chama tawala CCM.

Leo aliyekuwa M/kiti wa CHADEMA Wilaya Ngorongoro, Samweli Ole Nakumbale, aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2015, Elias Ngorisa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Ngorongoro, Wiliam ole Telele na wanachama wengine wa CHADEMA wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Wakitangaza uamuzi wao leo wamesema wanakwenda CCM kwani wameona kazi nzuri anayoifanya rais Magufuli hivyo na wao wameona ni vizuri kumuunga mkono wakiwa ndani ya Chama cha CCM.

Huu utakua ni muendelezo wa viongozi na wanachama wa CHADEMA kuhamia CCM. Kwani wiki kadhaa zilizopita tulishuhudia wanachama wa CHADEMA wakikihama chama hicho na kijiunga na CCM kwa sababu hiyo hiyo kuwa wanaridhishwa na kazi anayofanya Rais Magufuli.

You may also like