Aliyekuwa Diwani wa kata ya Gihandu Wilayani Hanang, Mkoani Manyara kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mathayo Samuhenda amejiuzulu udiwani wa kata hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Diwani huyo ameachia kiti hiko cha udiwani wakati akifanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Gihundi.

Kupitia mkutano huo amesema kwa muda wa miaka miwili sasa wananchi wa kijiji hiko wamekuwa na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kutokana na wanasiasa kutumia tatizo hilo kuombea kura.

”inatosha wanasiasa sisi tutumie shida ya maji ili tuombee kura, inatosha” amesema Samuhenda.

Hivyo amewaomba wananchi wa Gihandu kutosikiliza wanasiasa watakaokuja kuomba kura kwa kutumia tatizo hilo, amewaomba wasitoe kura kwa wanasiasa wa namna hiyo.

Gihandu amepokelewa na Mwenyekiti CCM, Mkoa wa Manyara, Lulu Simon ambaye naye alichukua nafasi hiyo kutoa neno kwa viongozi wa siasa na kuwaonya kuacha kufanya kampeni kwani wakati huu sio wakati wa kampeni.

Please follow and like us:
Pin Share