Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya teknolojia ya kilimo vijana nchini wametakiwa kuwasilisha bunifu zao za teknolojia ya kilimo ili kupata suluhu na kuongeza nafasi za ajira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu maalum ya kuwasilisha teknolojia hizo za kidigitali, Waziri  wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema lengo ni kuwavutia vijana wa Kitanzania katika kilimo cha kidigitali kwa kutumia teknolojia ili kuwaunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje.

Kuputia programu ya miezi mitatu vijana wenye bunifu mbalimbali za teknolojia ya kilimo watatuma bunifu zao kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Heifer International kwa kushirikiana na taasiai ya Sahara Venture ambapo mshindi wa kwanza atatunukiwa Sh milioni 20,mshindi wa pili Sh milioni 12 na watatu Sh milioni nane.

Amesema programu hizo zitaleta jibu la changamoto za wakulima wadogo hasa ikizingati kundi kubwa ni vijana.

“Sio kwamba vijana hawapendi kuingia kwenye kilimo,mifugo na uvuvi jambo la kwanza ni tatizo la ujuzi, pili ni mtaji namna ya kutekeleza katika mfumo wa biashara lazima kuwe na mitaji halafu jambo la tatu ni masoko.

Ameongeza “Umezalisha samaki kwenye bwawa lakini hakuna soko na kuna mahali watu wanahitaji utaunganishwaje?majibu ya haya yote ni teknolojia.”

Amesema kupitia programu hiyo watavutia kuwatafutia fursa na masoko ya uhakika hivyo wako tayari ili mradi wasivunje sheria.

Mkurugenzi Mkaazi wa Heifer International, Mark Tsoxo amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na wizara ya kilimo ambapo wanajihusisha maeneo ya vijijini kushawishi watu kulima kilimo cha kisasa.

“Hivi karibuni tumeaza kuangali sehemu kubwa ya vijana wa kitanzani ambao ni wengi hapa nchini ni asilimia 74 ya vijana na watoto hivyo hatuna budi kuwakwepa vijana tunamshuru Rais Samia kwa kuwa na programu hii kubwa ambayo inahusu vijana.”ameeleza.

By Jamhuri