Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza uteuzi na uhamisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, pamoja na mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kuwajumuisha Mawaziri kutoka ACT-Wazalendo.

Rais Dkt. Mwinyi ametangaza mabadiliko hayo leo, tarehe 03 Oktoba 2026, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu Zanzibar.

Katika mabadiliko hayo, ACT-Wazalendo imepata nafasi nne za uwaziri, ambapo:

  • Mhe. Nassor Ahmed Mazrui – Waziri wa Afya.
  • Mhe. Omar Said Shaaban – Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
  • Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar – Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
  • Mhe. Dkt. Mohamed Ali Suleiman – Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametangaza mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara, ikiwemo kuhamishia masuala ya Mipango Ofisi ya Rais, Ikulu, na kuanzishwa kwa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.

Mabadiliko mengine ni pamoja na: • Mhe. Shaaban Ali Othman – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Mipango na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.

  • Mhe. Masoud Ali Mohamed – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Uhusiano wa Jamii.
  • Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga – Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
  • Mhe. Ali Suleiman Ameir Mrembo – Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.

Kwa upande wa Naibu Mawaziri, mabadiliko yamefanyika katika Wizara mbalimbali, ikiwemo Afya, Kilimo, Elimu, Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Fedha, Utalii na Mambo ya Kale, pamoja na Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.

Rais Dkt. Mwinyi amesema mabadiliko hayo yanaendelea kutekeleza makubaliano ya maridhiano baina ya CCM na ACT-Wazalendo kuhusu uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Mawaziri na Naibu Mawaziri wote walioteuliwa na waliohamishwa wataapishwa Jumatatu, tarehe 05 Oktoba 2026, saa 8:00 mchana