Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kufanya ziara ya Kitaifa nchini India Oktoba 8 hadi 1, 2023 akiambatana na wafanyabiashara kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji kiuchumi.


Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Januari Makamba ambapo amesema Rais atawasili nchini India /Oktoba 8 na siku inayofuata ya tarehe 9 atapokelewa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa India.

Waziri Makamba amesema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ya Rais Dkt Samia ni kukukuza ushirikiano wa kidiplomasia yakiuchumi baina ya Tanzania na india katika sekta za ikiwemo ulinzi, maji, kilimo, afya, biashara na uwekezaji.

” Moja ya mashirikiano yetu na nchi ya India ni katiks sekta ya afya kwani imefanikiwa sana kwa sekta hiyo hivyo kupitia ziara hiyo tutaanzisha taasisi ya upandikizaji figo pia kiwanda cha kutengeneza chanjo za binadamu na wanyama, na Kuboresha utaalamu katika sekta ya ikiwemo , upatikanaji wa dawa katika uboera na weledi amesema Waziri Makamba.

Waziri Makamba abainisha kuwa katika sekta ya kilimo ziara italeta fursa ya kukuza masoko ya mazao ya kilimo ikiwemo mbaazi, korosho na kuhakikisha soko hilo linaendelea kuwepo na kuongezeka pia kuanzisha kongamano la viwanda ndani ya Tanzania.

Pia amesema kwa kuwa nchi ya India imeendelea katika sekta ya maji hivyo italeta uanzishwaji wa karakana utengenezaji wa vyombo vya usafiri majini kwani Tanzania kuna mradi wa maji wa ziwa Victoria bahari .

“Mikataba 15 ipi katika mazungumzo yatakapofikia muafaka itasainiwa kati ya Tanzania na india kuweka ushirikiano katika kutekeleza Diplomasia yauchumi kutafuta masoko na kuimarisha uwekezaji” amesema Waziri.

Aidha matukio atakayofanya Rais Dkt Samia ni ikiwemo kwenda kuweka shahada la maua katika kaburi la mtu aliyekuwa mashuhuri nchini India Indira Ganzi pia atafanya mazungumzo ya faragha na Waziri Mkuu wa India atafanya mkutano na waandishi wa habari Kisha kukutana na wafanyabiashara waku wa katika kongamano.