Rais wa Kenya, William Ruto kesho ataanza ziara ya siku mbili nchini, tangu alipoapishwa Septemba 13, mwaka huu kuwa rasi wa tano wa nchi hiyo.

Tangu alipoapishwa, Rais Ruto ametembelea nchi tatu tofauti, ikiwamo Uingereza alikokwenda kuhudhuria maziko ya Malkia Elizabeth II, Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa na jirani zake wa Ethiopia.