Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani

Rais Samia Suluhu Hassan,amegawa ardhi hekari 5,520 kwa Wananchi wa Wilaya za Bagamoyo na Kibaha.

Hayo yamesemwa na David Silinde Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa makabidhiano ya ardhi  iliyokuwa sehemu ya Ranchi ya Ruvu kwenda kwa Wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo na Kibaha ambapo pande zote zimeridhia.

Ameeleza uamuzi huo wa  Serikali ni kuwawezesha Wananchi kupata Ardhi kwa ajili ya Shughuli za kilimo, Mifugo na shughuli zingine za kijamii.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ranchi ya NARCO Ruvu ukishuhudiwa na Viongozi wa Wilaya,Tarafa, Kata, Vijiji na Viongozi wa Wakulima na Wafugaji na wawakilishi wa Wananchi kutoka Vijiji 10. 

Akipongeza uamuzi , Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewaagiza Viongozi wa Mkoa na Wilaya kutimiza wajibu wao wa kusimamia kupanga matumizi ya Ardhi.

Pia Kunenge amewataka Wananchi kuheshimu Sheria na kwamba wasivamie eneo hilo la Serikali.

By Jamhuri