Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu HassanĀ  akiwa kwenye mazungumzo na Mwimbaji Maarufu wa Muziki wa Jamhuri ya Korea Cho Yong-pil, Jijini Seoul, tarehe 03 Juni, 2024. Mwimbaji huyo Maarufu ameimba nyimbo mbalimbali ikiwemo baadhi za kutangaza vivutio vya Utalii nchini Tanzania.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu HassanĀ  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwimbaji Maarufu wa Muziki wa Jamhuri ya Korea Cho Yong-pil mara baada ya mazungumzo yao Seoul, tarehe 03 Juni, 2024. Mwimbaji huyo Maarufu ameimba nyimbo mbalimbali ikiwemo baadhi za kutangaza vivutio vya Utalii nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Mwimbaji Maarufu wa Muziki wa Jamhuri ya Korea Cho Yong-pil wakati wa mazungumzo yao Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya DVD zenye nyimbo za vivutio vya Utalii nchini Tanzania kutoka kwa Mwimbaji Maarufu wa Muziki wa Jamhuri ya Korea Cho Yong-pil wakati wa mazungumzo yao Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03 Juni, 2024.