Balozi Rupia (86) amefariki leo asubuhi nchini Afrika Kusini ambapo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kama ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje katika nchi mbalimbali.

Pia, aliwahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Dar es Salaam.