Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi milioni 500 kwa ajili ya Mashindano yanayohusu Timu za Taifa za Tanzania kutoka kwa Mfanyabiashara Said Naseer Naseer kwa niaba ya Wafanyabiashara wenzake kutoka Zanzibar. Shughuli hii imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia mfano wa Hundi ya Shilingi milioni 500 kwa ajili ya Mashindano yanayohusu Timu za Taifa za Tanzania Ikulu Jijini Dar es Salaam. Fedha hizo zimetolewa na Wafanyabiashara wa Zanzibar katika kumuunga mkono Rais Samia kwenye michezo tarehe 04 Aprili, 2024. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishuhudia


By Jamhuri