Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kushiriki zoezi la ujazaji maji katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lililopo Rufiji Mkoani Pwani leo Desemba 22, 2022

Bwawa la umeme la Julius Nyerere linalojengwa kati ya Mkoa wa Pwani na Morogoro likigharimu takribani shilingi Trilioni 6.5 linatarajiwa kujazwa kwa lita ujazo bilioni 33 ikiwa ni mara 10 ya bwawa la Mtera lenye lita za ujazo bilioni 3.7 na linatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115.