Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023. Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho nchini India. Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.