Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Wachezaji Sarakasi wa Kimataifa, Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu maarufu kama Ramadhani Brothers baada ya kuibuka Mabingwa wa Dunia katika Mashindano ya America’s Got Talent Fantasy League.

“Pongezi kwa vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League. Safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine.” ameandika Dkt Samia kupitia ukurasa wake wa instagram.

Kufuatia ushindi huo Ramadhani Brothers wamevuna kitita cha Dola za Kimarekani 250, 000 sawa na Milioni 640 za Kitanzania, nawameingia kwenye rekodi ya kuwa Watanzania wa kwanza kushinda AGT katika historia ya mashindano hayo.

By Jamhuri