Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro tayari kwa kuelekea mkoani Arusha ambapo ni mgeni rasmi kwenye Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kitakachofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Agosti 28, 2024.


Dkt. Samia amewasili uwanjani hapo akitokea nchini Kenya ambapo alihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), tarehe 27 Agosti, 2024

Please follow and like us:
Pin Share