Akiongea katika Ikulu ya Marekani, Rais Trump ameutambua mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel, maamuzi ya kihistoria yanayopindua sera za miaka mingi za Marekani.

Rais Donald Trump ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati.

Trump amesema yuko tayari kutafuta suluhu katika mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina ikiwa pande zote mbili zitataka. Awali maofisa wa marekani walikuwa wameeleza kuwa Rais Trump angeutambua tu ukweli kuwa Yerusalem inahudumu kama mji mkuu wa Israel ijapokuwa Wapalestina nao wanautambua mji huo kama mji wao mkuu.

Kwa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, Marekani itakuwa inaenda kinyume na sera yake ya muda mrefu kwamba hatima ya mji huo mtakatifu inafaa kuamuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.

By Jamhuri