Na mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Leo Oktoba 18, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amekutana na wadau wa usafirishaji katika mkutano maalum uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Arnatoglo Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.

Chalamila amewashuru wadau hao kwa kazi nzurii wanazoendelea kufanya vilevile amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika sekta ya usafirishaji na namna anvyoifungua sekta hiyo kwa sasa usafiri upo masaa 24.

Aidha Chalamila amesema wadau wa usafirishaji ni kundi muhimu hakuna anayeweza kubeza ukweli huo, na uwekezaji wowote unaofanywa lazima uwe na tija lakini popote wanapokutana na Changamoto njia ya mazungumzo iwe kipaumbele na sio migomo.

Pia Chalamila alipata wasaa wa kusikiliza maoni na Changamoto zinazoikabili sekta hiyo ambapo kwa sehemu kubwa inatokana na kupanda kwa gharama za mafuta ambapo walio wengi katika mawasilisho yao wameiomba Serikali kupandisha nauli ili waweze kupata faida angalao kuliko ilivyo Sasa.

Hata hivyo Chalamila ameitaka mamlaka husika LATRA kukaa pamoja na kujadili kwa kina Changamoto hiyo na kuipatia majawabu lakini ni vizuri maamuzi yatakayo fanyika yazingatie pia hali halisi ya uchumi wa wananchi.

Kwa upande wa Baraza la LATRA wamesema Changamoto zinazoikumba sekta ya usafirishaji ni kwa sababu ya kutumia nishati ya mafuta pekee ni wakati muafaka wa kuangalia fursa zingine ikiwemo kuanza kutumia nishati mmbadala ikiwemo gesi katika vyombo vya usafiri kwa kuwa utaalam huo kwa sasa upo hapa nchini.

By Jamhuri