Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa taarifa kwa umma, leo Machi 25, 2024 kupitia vyombo vya habari Ofisini kwake Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila amesema ndege mpya ya abiria aina ya Boieng B737-9 Max ya Shirika la Ndege ATCL inatarajiwa kuwasili nchini ambapo ndege hiyo inauwezo wa kubeba abilia 181 itawasili kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere Dar es Salaam (JNIA)

Aidha RC Chalamila ametoa rai kwa Watanzania wote hususani wakazi wa Dar es Salaam, viongozi mbalimbali kuja kwa wingi kushuhudia mapokezi hayo.

Mwisho RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa za kuwekeza katika Sekta ya Anga, ndani ya miaka mitatu madarakani tayari ameshanunua ndege 3.