Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime

Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda amewataka Waandishi wa Habari kufanya kazi bila wasiwasi wakihofia Usalama wao katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika kikao na waandishi wa habari na maafisa habari kilichofanyika mkoani Mara amebaini waandishi kuwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za kiusalama.

Amewataka waandishi kutimiza wajibu wao kwa kuandika habari kwa weredi juu ya mabaya na mazuri japo ukweli unauma na una umiza na sio wote wanakubali ukweli uandikwe.

Kwa upande wake amesema yeye haogopi ukweli kwani hupata fursa ya kufanyia kazi upya katika utendaji kazi wa nafasi yake ya uongozi na kuongeza kuwa anapenda kuona habari za uchunguzi pamoja na Waandishi wanaojitegemea kutafuta habari.

Akiendelea kuzungumza amewataka viongozi wa ima kuacha mara moja tabia ya kukwamisha utoaji habari kwa Waandishi na kuwataka waandishi watakao kumbana na changamoto hiyo wajulishe.

By Jamhuri