Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia,Kibaha

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewaasa watumishi wa Umma kuacha tabia ya kusemana hovyo ,kuwekeana fitna ,na kufanyiana vituko kwani kwa kufanya hivyo ni kuzorotesha utendaji kazi kwenye maeneo yao.

Aidha amewataka watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa kuleta tija na kuacha alama.

Akizungumza na watumishi wa Serikali Mkoani Pwani pamoja na Halmashauri ya Kibaha Mjini , Ridhiwani alitaka , kila mmoja kutimiza wajibu wake na kuwa wabunifu kwenye utendaji kazi wao.

“Naelekeza kuacha kasumba ya kusubiri kushurutishwa na kusimamiwa kwenye majukumu yao ya kazi,bila kujituma wenyewe, kuna watumishi ambao wao wana

Vilevile aliwataka maofisa Utumishi wabadilike katika utendaji kazi wao ili kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa watumishi.

“Hili ni eneo muhimu ,shughulikieni matatizo ya watumishi,ondoeni malalamiko ya Utumishi na kuwashauri kama Kuna sintofahamu ili kushirikiana na kuweza kufanya mambo yaende vizuri” amesema.

Kuhusu Malimbikizo, Ridhiwani alifafanua malimbikizo ya mishahara yanaendelea kufanyiwa kazi na ipo fedha ambayo wote watalipwa kulingana na taratibu zilizowekwa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge aliwataka watendaji na watumishi kufanya kazi zao kwa kutekeleza utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Amesema wana wajibu wa kutekeleza mipango ya maendeleo na kuondoa kero za wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani hiyo.

Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta alieleza watumishi waliopo ofisi ya mkoa na wilaya ni 189 na upungufu ni 137.

Kwa upande wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Mshamu Munde amesema watumishi waliopo ni Zaidi ya 2,400 na kuna upungufu wa watumishi 144.

By Jamhuri