Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA

Kocha mkuu wa wekundu wa msimbazi Simba SC  Robert Oliviera ‘Robertinho’ amesema kwasasa anataka kucheza hatua ya robo fainali ya michuano Klabu Bingwa  Barani  Afrika.

Robertinho ameyasema hayo baada ya kufumua hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuifunga mabao 7-0 Horoya ya nchini Guinea, Machi 18 mwaka huu katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam.

Robertinho amesema kwanza kabisa anafuraha kubwa kufuatia kuwa sehemu ya makocha walioifikisha Simba SC Robo Fainali ya michuano ya CAF, na sasa malengo yake anayaelekeza kufikia Hatua ya Fainali.

“Ninashukuru Mungu hivi sasa kila mmoja anaona mabadiliko yaliyokuwepo ya timu, hivi sasa inacheza soka safi la pasi sambamba na kupata ushindi mzuri.”
“Hiyo inanifanya nifikirie kufika katika hatua ya fainali ya michuano hii mikubwa Afrika, kwani nina amini ubora wa kila mchezaji wangu nitakayempa nafasi ya kucheza,” amesema Robertinho.

Ameongeza kuwa anapata jeuri kutokana na kikosi chake kuimarika zaidi ya kadiri siku zinavyokwenda kwa wachezaji wake kucheza kwa kufauata maelekezo yake na kupata ushindi.

“Kama unakumbuka vizuri, wakati nakabidhiwa niliomba muda wa kutengeneza timu itakayokuwa na muunganiko wa wachezaji watakaokuwa bora.”

Ushindi wa magoli 7-0 dhidi ya Horoya umeifanya Simba SC washike nafasi ya pili katika Msimamo wa Kundi C ikiwa na alama 09 huku Raja Casablanca ikiongoza Kundi hilo kwa kuwa na alama 13, zote zikicheza michezo mitano.

By Jamhuri