Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia,Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara l ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa Habari za Mazingira (JET) wamewataka wanahabari kuendelea kutoa elimu juu ya utatuzi wa migogoro ya binadamu na wanyamapoli kwa jamii kwa kwenye sehemu zenye shoroba.

Akizungumza na Jamhuri Mkurugenzi mkuu wa JET John Chikomo ,mara baada ya mdahalo wa waandishi wa habari na wataalamu kwenye mdahalo ulioandaliwa na  Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa Mradi wa Kupunguza Migongano Baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania, unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani kwa ufadhili wa (BMZ) amesema kuwa madhumuni ya mdahalo huo ni kuongeza uelewa kwenye habari zinazohusu wanyamapori.


Chikomo amesema mkutano huo ni muendelezo wa utoaji elimu kwa Waandishi wa Habari kwenye mradi wa uhifadhi hasa kwenye kupunguza migogoro baina ya Wanyamapoli na binadamu nchini.

John Chikomo amesema mikakati iliyopo kwa sasa, ni kuhakikisha mradi wa kuondoa migogoro baina ya binadamu na wanyamapori unakuwa na matokeo chanya.

“Sisi kama JET tupo kwenye kuwajengea uwezo waandishi wa habari, waweze kutoa elimu kwa jamii juu ya kuepuka migogoro ya binadamu na wanyapoli na mwisho tutawawezesha waende kwenye shoroba na Wananchi na wadau mbali mbali wanaoshiriki masuala ya uhifadhi na mwishowe kutoa habari zinazohusu Wanyamapoli”amesema .

Amesema kwa sasa mradi huo upo kwenye mikoa ya Lindi kwa maana ya Liwale na Ruvuma wilaya za Tunduru na Namtumbo na kwa upande wa elimu ya hewa ukaa mikakati iliyopo ni kutoa elimu kwa Waandishi kwani ina manufaa kwa jamii JET mpaka sasa wameweza kufundisha waandishi 25 wa mikoa inayozunguka maeneo ya mradi.


Forunatha Msofe Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyamapoli ,Wizara ya Maliasili na Utalii amesema lengo kuu ni kuzungumzia utatuzi wa migongano baina ya binadamu na Wanyamapoli hasa kwenye ukanda wa Ruvuma.

Amesema tangu 2021 katika eneo wameanzisha, mradi wa utatuzi wa migogoro ya Wanyamapoli na binadamu kwa kushirikiana Jamhuri ya Ujerumani.

Afisa Mtafiti Mkuu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Stephen Nindi akitoa maelezo ya namna serikali ilivyoshiriki katika kukabiliana na Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori katika ukanda wa Ruvuma.

“Mradi wa kitaifa 2020 na 2024 umejikita katika kuwezesha watumishi wa wizara, kuhakikisha unatekeleza ili matokeo yake yaweze upelekwa kwenye kanda zingine za kitaifa .

Lakini kupitia halmashauli za wilaya Namtumbo, Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma, na Liwale mkoani wa Lindi tutahakikisha ma ofisa Wanyamapoli wa wilaya na Askari wa vijiji wanaweza kusadia kuzuia matukio yanayotokana na usimamizi wa Tembo kwenye makazi ya watu yanashughulikiwa haraka na taasisi zetu za TAWA na TANAPA”amesema.

Amesema katika mradi huo watahakikisha ma Ofisa Wanyamapoli na askari wa kijiji katika maeneo yote ya uhifadhi wanakuwa na vitendea kazi kwa ajili ya kushughulikia changamoto zinapotokea .

“Kwa kipindi cha miaka mitatu tunajenga mfumo ambao utaweza kufanya kazi ,lakini baada ya kufanya kazi vizuri tutaweza kuunganisha kwenye wilaya zote zenye migogoro ya Wanyama na binadamu
Pia kuhakikisha Wanyapoli haswa Tembo, hawaleti madhara kwa jamii ,hivyo wanaweza kurejeshwa hifadhini kabla hawajaingia kwenye maeneo ya vijiji na mashamba ya watu.’’ameongeza .

Fortunatha amesisistiza wananchi kushirikiana washirikiana ,kutoa taarifa pale wanapo ona kuna wanyamapori ,ambao wameingia kwenye maeneo yao kupitia askali wa vijiji na TAWA na TANAPA.


Amesema matumizi bora ya ardhi kwa kiasi kikubwa yanazingatia uokoaji wa Shoroba kubwa, unao julikana kama Seloou Nyasa ambao umezungukwa na maeneo ya hifadhi za jamii zinajukalina kama BMA.


“Tukapozingatia mipango ya matumizi bora tusiwe tuna lima maeneo ya Wanyamapoli, ambayo ni ya hifadhi tutahakikisha Tembo hawaingii kwenye maneneo ya wakazi na mashamba ambayo yana jumuisha mapito ya Wanyamapo kupanda mazao ambayo haya wavutii” amesema.

Meneja Mtekelezaji wa Mradi huo kutoka GIZ, Cristina Georgii

Mwenyekiti wa JET, Dk Ellen Otaru amesema suala zima la ya udhibiti baina ya binadamu na wanyama poli ,waandishi wa habari wananafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kwa kutumia lugha rafiki yenye kueleweka haraka na jamii .


Amesema mwandishi wa habari ni mtaalamu wa kuchambua miongozo mbalimbali ya sheria na kuiweka katika lugha nyepesi , kuliko mwananchi wa kawaida sasa toeni elimu kupitia vyombo vyenu jamii ielewe haraka.


Dkt Hellen ameongeza kuwa kupitia karamu za wanahabari , kila Mtanzania ataelewa nafasi yake ,kwenye suala zima la uhifadhi kwa sababu jamii inawajibu kwa kusaidia kuondoa migogoro ya binadamu na wanyamapori.