Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) , Mhe. Prof. Adolf Mkenda (mb) akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari Bungeni jijini Dodoma.

………………………..

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) , Prof. Adolf Mkenda (mb) amesema kuwa suala la kuangalia upya ajira za walimu ni maboresho ya Sera za Kitaifa toka kwa wadau ili kudhibiti ubora wa sekta ya elimu nchini, leo Jumanne, tarehe 20 Juni 2023 wakati akifanya mahojiano na Vyombo vya habari nje ya ukumbi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jijini Dodoma

Prof. Mkenda amefafanu kuwa Wizara ya Elimu imechukua takribani mwaka mzima kuratibu zoezi la ukusanyaji maoni, hoja na mapendekezo ili kuhakikisha tunapata walimu bora na sio bora walimu.

“Katika Mapendekezo ya Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2020/2023 , na Sera itakapopita ndio utaratibu mpya, suala la msingi hapa ni walimu wapya ndio watapitia utaratibu huu wa kuchujwa kwanza na ni utaratibu wa kawaida ambao upo kwa fani tofauti kama vile madaktari na wanasheria ni muhimu kwa mstabali wa Taifa maana ndio wanatufundishia kada nyingine zote” alisisitiza Prof. Mkenda

Aidha, Prof. Mkenda aliongeza tamko la kisera liliratibiea kuoitia uendeshaji wa semina mbalimbali za ushiriki wa waheshimiwa wabunge pamoja na walimu pia, Prof Mkenda amesema kuwa baada ya Sera hii kupita itasaidia kurasmisha kada ya ualimu na kuhakikisha kila mwalimu atakaepata ajira atakuwa ni mwalimu bora kwa kupitia vigezo vyote muhimu vitakavyoainishwa kupitia mchakato huu

“Rasimu hii ishapitia hatua zote muhimu na natumaini kama ikipita kwenye baraza la mawaziri mwezi wa 9 itakuwa tayari kupitia baraza hili ambalo kimsingi ndio linalomshauri Mhe Rais kuhusu uwepo wa tamko la uendeshaji Mitihani kwa walimu wapya wanaojiunga na ajira hizo nchini” alisema Prof Mkenda

Vilevile, Prof Mkenda alitoa rai kwa wanachi kubadili dhana na mtazamo wa kuheshimisha kada ya ualimu kama zilivyo kada nyingine na isiwe ni Kimbolio la waliokosa ajira nchini.

“Nirudie kusema tena , utekelezaji utafanyika baada ya tamko hili la kisera kupitishwa kutakuwa na kanuni na nafasi ya kushirikisha tena wadau , Nitoe rai kwa waalimu waliopo makazini tunatenga bajeti ya kuwaendeleza na hatutawaondoa kazini na ajira zao zitabaki kama zilivyo mpaka watakapo fikia umri wa kustaafu” alihitimisha Prof Mkenda.

By Jamhuri