Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka kwenye boti katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya
Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakati wa ziara yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza Faiswary.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa Chifu wa kitongoji cha Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili, kata ya Lupingu, Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya pongezi kwa kiongozi wa kitaifa kufika hapo tangu mwaka 1979 katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa miwani ni Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nsele kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Mzee Kolimba akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
 
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa ajili ya kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za Ziwa hilo
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kukagua bandari za Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi bandari ya Itungi iliyopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Katik ziara hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetenga fedha hizo kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa waliojitolea maeneo yao ili kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari zilizopo ndani ya Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Lipingu iliyopo Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe hadi bandari ya Matema iiyopo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Naye Mkuu wa Wilaya wa Ludewa Bwana Andrea Tsere amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa tayari wamekamilisha kazi ya kuhakiki malipo ya fidia za wananchi waliotoa ardhi zao eneo la Manda na Lupingu. “Wanachi wa eneo la Manda watalipwa shilingi milioni 192 ambapo wametoa eneo la ukubwa wa hekari 24 na wa Lupingu wametoa eneo ukubwa wa hekari 10.6 na watafidiwa shilingi milioni 166, amesema Tsere”.
Bwana Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania inakamilisha ujenzi wa meli ya mizigo na abiria na itaanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo ndani bandari za Ziwa Nyasa mwezi Agosti mwaka huu ambapo meli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria mia mbili na mizigo tani mia mbili kwenye jumla ya bandari kumi na tano zilizopo ndani ya mwambao wa ziwa Nyasa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa amemshukuru Mhe. Mhandisi Nditiye kwa niaba ya wananchi wake kwa kufika kwenye makazi ya wananchi hao waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa na kukagua mahitaji ya usafiri wa majini wa abiria na mizigo wa Ziwa hilo ambapo Serikali tayari imetenga fedha kulipa fidia wananchi waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi na upanuzi wa bandari za Ziwa hilo.
Ujenzi wa bandari hizo na utoaji wa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo ni ukamilishaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ambao wanategema Ziwa hio kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za kiuchumi, biashara na kijamii ambazo zitachangia ukuaji wa uchumi wa wananchi hao na taifa kwa ujumla.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano

By Jamhuri