Serikali imesema itaendelea kuwaunga mkono vijana wanaobuni teknolojia mbalimbali zinazosaidia katika kutatua changamoto za mazingira zinazoikabili nchi yetu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo wakati akifungua Kongamano la Bunifu katika Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi lililofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Amesema changamoto za mazingira hasa ukame unayoyakabili baadhi ya maeneo nchini pamoja na usimamizi wa taka ngumu zinakwenda kutatuliwa kupitia vijana wanaojikitika katika kubuni nyenzo rafiki wa mazingira.

Serikali imesema itaendelea kuwaunga mkono vijana wanaobuni teknolojia mbalimbali zinazosaidia katika kutatua changamoto za mazingira zinazoikabili nchi yetu.

Dkt. Jafo ametoa rai kwa vijana kutumia fursa ya kukusanya taka ngumu na kutengeneza bidhaa mbalimbali hatua itakayowapatia ajira na pia kusaidia katika shughuli ya utenganishaji wa taka.

“Tunaelezwa hapa, nchi yetu inazalisha mamilioni ya tani za taka ngumu kwa mwaka na kati ya hizo ni asilimia 30 tu ndizo zinaingia katika mfumo rasmi wa uchakataji hivyo teknolojia hizi vijana mlizobuni zitasaidia sana katika utunzaji wa mazingira, niwaombe muendelee kujikita katika teknojia ya recycling (urejelezaji) ya taka,” alisema

Aidha, Waziri Jafo aliwahimiza vijana kuchangamkia fursa ya Biashara ya Kaboni ili si tu kujipatia kipato bali pia kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhifadhi mazingira kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aliweweka wazi kuwa kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) hadi kufikia Julai 2023 tayari miradi 25 imekwishasajiliwa hivyo aliwahimiza vijana kuchangamkia fursa hiyo.

Hali kadhalika Dkt. Jafo ametoa wito kwa Asasi ya Anza iliyoandaa kongamano hilo kuendelea kuwasimamia vijana hao waweze kukua zaidi na waje kuonesha mafanikio makubwa zaidi katika teknolojia bunifu rafiki kwa mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknolojia wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. Gerald Kafuku amesema wanaendelea kuratibu, kuendeleza na kusaidia vijana katika teknojia.

Amesema Tume inawasadia wabunifu kifedha na kiutaalamu ambapo imetoa shilingi bilioni 1.4 kwa wabunifu 37 na kuviwezesha vikundi vya ubunifu vitano kupitia programu maalumu iliyoianzisha.

Bw. Kafuku amesema kuwa tayari miradi minane ya teknokojia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kujenga mazingira wezeshi kwa wabunifu wa magari na pikipiki zinazotumia umeme badala ya mafuta.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati akifungua Kongamano la Bunifu katika Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi lililofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Agosti, 2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Anza Bw. Joshua Elias amesema kuwa lengo la ubunifu huo ni kubadilisha taka ambazo zingeweza kuwa na athari za kimazingira na kuzibadilisha kuwa fursa.

Ameendelea kueleza kuwa, kupitia ubunifu huo vijana wataweza kuingiza bidhaa hizo sokoni na kutatua changamoto za uchafuzi wa mazingira na wakati huo kuwaletea ajira.

Hivyo, kupitia kongamano hilo ambalo limeandaliwa na asasi anayoingoza, Bw. Joshua aliishukuru Serikali kwa kuunga mkono juhudi za vijana wanaojikita katika ubunifu.