Serikali inayoondoka madarakani imeanza maandalizi ya kuikabidhi madaraka serikali ijayo,huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) ikiendelea na mchakato wa kujumlisha kura .

Joseph Kinyua,Mkuu wa huduma za umma amesema wakati wa mkutano wa kamati inayosimamia makabidhiano ya mamlaka mapema leo kuwa wako tayari kufanikisha makabidhiano ya mamlaka kwa mujibu wa sheria.

Kinyua alikuwa akizungumza katika jengo la Harambee House akiambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ambao ni pamoja na Mwanasheria mkuu Paul Kihara, Mkuu wa majeshi Robert Kibochi,Inspekta Mkuu wa Polisi Hilary Mutyambai, Katibu wa kudumu wa wizara ya mambo ya ndani Karanja Kibicho na Katibu wa kudumu wa wizara ya mambo ya nje Macharia Kamau.

Kinyua alisema kuwa jukumu la kamati hiyo litaanza mara tu baada ya mshindi wa urais kutangazwa.

Zinazohusiana

Fuatilia matokeo ya awali ya uchaguzi Mkuu Kenya

Endelea kufuatilia matokeo ya uchaguzi Kenya

Tume ya Kenya iliarifu kwamba takribani asilimia 65 ya wakenya zaidi ya Milioni 12 waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne Agosti 9, 2022 kuchagua wawakilishi na zoezi la kuhesabu kura linaendelea mpaka pale tume hiyo itakapotangaza mshindi wa kinyang’anyiro cha urais.

Na ushindani unaonekana kuwa mkali kutokana na wagombea kutoka Chama cha Azimio Raila Odinga na UDA William Ruto kuchuana vikali katika matokeo ya awali .

By Jamhuri