Serikali imeondoa zuio la kuuza mazao nje ya nchi ili kutoa fursa soko na mapato kwa wakulima.

Hata hivyo, wanaotaka kuuza mazao nje ya nchi watalazimika kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Agosti 8 na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwa akiyafunga rasmi maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

“Hata hivyo, lazima kila mwananchi kuanzia ngazi ya kaya kuhakikisha uwepo wa akiba na usalama wa chakula,” amesema Mkapa

Amewataka Watanzania kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo inayoajiri zaidi ya asilimia 65 ya watu nchini ili kuvihakikishia malighafi viwanda vinavyoendelea kujengwa kutekeleza sera ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Please follow and like us:
Pin Share