Siku ya Sikukuu ya Krismas klabu ya Yanga itakuwa wageni wa Azam pale Uwanja wa Mkapa katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2 katika mechi ya mzunguko wa kwanza. 

Mechi hiyo ilitarajiwa kuwa na presha kubwa kwa Yanga kwa sababu ya tofauti ya pointi iliyokuwa kati yao na wapinzani wao wa karibu Simba SC na Azam wenyewe lakini baada ya matokeo ya sare ya Simba na Azam dhidi ya Kagera Sugar ni wazi kwamba wameipata Yanga uhuru mkubwa kileleni mwa ligi huku wanajangwani hao wakiwa juu kwa tofauti ya pointi 6 dhidi ya Yanga na point 7 dhidi ya Azam. 

Yanga wataingia uwanjani kwa utulivu kwa sababu matokeo yeyote mabaya hayatawaathiri sana tofauti na awali ambapo pengo lao dhidi ya Simba lilikuwa ni pointi 4 pekee na ikiwa wangepoteza au kutoa sare basi wangetoa upenyo kwa wapinzani wao kuwakaribia zao na kuweka rehani matumaini ya ubingwa. 

Mpaka sasa Yanga SC wana point 44 wakifuatiwa  na Simba na Azam wenye point 38 na 37 hali inayowapa uhakika wananchi kuingia mwaka mpya wakiwa wanaongoza ligi na watakwenda katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi wakiwa kifua mbele. 

Baada ya Yanga kupata kipigo cha 2-1 toka kwa Ihefu SC mashabiki wengi wa soka waliamini Simba itaendelea kuipa Yanga presha kwa kushinda mechi zao huku wakiisubiri Yanga ipoteze mechi nyingine lakini mambo yamekuwa magumu Kaitaba na kuifanya Yanga iondoke katika presha ya kufukuziwa na Simba kwa ukaribu.

By Jamhuri