Na Isri Mohamed

Klabu ya Simba imemtambulisha mlinda lango wao mpya, Moussa Camara (25), Rais wa Guinea akitokea klabu ya AC Horoya ya nchini Guinea.

Simba imesajili nyanda huyo kuchukua nafasi ya golikipa wao namba mopja, Ayoub Lakred, ambaye atakuwa nje kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha aliyoyapata wakiwa nchini Misri kwenye pre Season.

Camara alianza kucheza soka kwenye timu ya vijana ya FC Kolombada katika madaraja ya chini

Baadae alijiunga na klabu ya daraja la pili ya Milo FC na mwaka 2015 akasajiliwa Horoya AC alipodumu mpaka kwenda Simba.

Simba sasa itakuwa na jumla ya magolikipa watano, Ayoub Lakred, Aishi Manula, Ally Salim, Hussein Abel na Moussa Camara.