Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Mkurugenzi Mtendaji wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Godfrey Malekano amesema kuwa watendelea kuimarisha mifumo katika utendajikazi wa taasisi hiyo ili kuongeza mchango katika kuchochea uchumi wa Tanzania.

Ameyasema hayo leo Septemba 6,2023 jijini Dar es Salaam wakati mkutano na wahariri na waandishi wa habari kuhusiana na utendajikazi wa taasisi hiyo.

Amesema kuwa wataimarisha zaidi mfumo wa stakabadhi za ghala, na ushiriki wa vikundi vya wakulima ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ili kuwafikia wadau wengi nchini.

Malekano amesema kazi ya kujenga mfumo imara wa soko la bidhaa inategemea mchango wa Serikali taasisi na sekta binafsi hivyo ushirikiano ni muhimu kufikia adhma hiyo.

Amesema kuwa kwa sasa soko hilo linafanya mauzo ya papo kwa papo huku lengo likiwa ni kuanzisha mauzo ya mkataba pale miundombinu itakaboreshwa na kuongeza kuwa soko hilo linasaidia taarifa za ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa utoaji wa vibali kwa usafirishaji wa bidhaa pamoja na upatikanaji wa fedha za kigeni.

Pia amesema kutokana na kuipa kipaumbele sera ya soko la pamoja la Afrika hivyo ni muhimu kuzingatia viwango vinavyofanana ili kuboresha biashara kati ya nchi na nchi ndani ya Afrika.

Alisema juhudi zilizofanyika hadi sasa ni kuendelea kuboresha mfumo wa kielektroniki ili kuongeza bidhaa zaidi kwa ajili ya mauzo.

Pia amesema kwa sasa mfumo wa kielektroniki wa TMX unaweza kuhusisha ‘reverse actions’ ambapo wanunuzi wanaweza kutangaza kununua kiasi fulani cha bidhaa ya daraja maalum katika eneo maalumu la kuwasilisha na wauzaji kushindana kwa bei kwenye mfumo wakati wa mauzo.

Kuhusu faida ya soko kwa upande wa serikali ” Ni njia rahisi ya kukusanya mapato kwa Halmashauri, upatikanaji wa taarifa za kuaminika,ni njia rahisi ya ukusanyaji mapato ya taasisi husika, urahisi wa usimamizi wa utoaji wa vibali husika kwa usafirishaji wa bidhaa zilizouzwa”

“Muda zaidi kwa wadau wengine kujikita katika kuboresha uzalishaji wa mazao, Kuhamasisha kampeni ya uchumi wa viwanda, kusaidia upatikanaji wa fedha za kigeni, na kusaidia biashara ya Kimataifa kwa gharama nafuu (AFCFTA).

Faida za soko la bidhaa Tanzania kwa upande wa mteja, mnunuzi atakua na uwezo wa kupata mazao mengi na yenye ubora kwa wakati mmoja, kupunguza gharama (muda na fedha), kupunguza athari mbalimbali yaani kwenye ubora na wizi, upatikanaji wa taarifa za soko, na kujikinga na mabadiliko hasi ya bei.

Kwa upande wa mkulima au muuzaji, atanufaika na soko hilo kwa kuimarisha bei ya soko, upatikanaji wa taarifa za soko, kuongeza kwa ufahamu wa uzalishaji bora, uhakika wa malipo, na mkulima kuwa huru kuamua bei aliyoridhia bidhaa zao.

Amesema, soko la Bidhaa Tanzania ni mfumo rasmi unaokutanisha wauzaji na wanunuzi kwa pamoja na kufanya biashara ya mkataba inayotoa uhakika wa ubora, ujazo na malipo hivyo ili kupata mafanikio makubwa inahitaji uwekezaji wa kisasa wa maghala.

“Mchakato wa kuanzisha soko la bidhaa ulianza muda mrefu, mwaka 2009 wakati wa udinzudi wa ule moango wa kilimo kwanza ambapo mazungumzo makubwa yalikuwa ni kuongeza uzalishaji wa mazao.

“Ikaonekana kwambza zaidi ya kuongeza uzalishaji kuna suala la masoko, Soko la Bidhaa ikatahwa kama moja ya jambo muhimu, kazi ikaanza mwaka 2012 kwa kupata baraka za Baraza la Mawaziri mwaka 2014,” amesema.

Amesema kuwa, mradi wa kuanzishwa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) ulizinduliwa Novemba 30,2015 na Rais Mstaafu wa Awamu ya NNe, Dkt. Jakaya Kikwete.

“Sheria ya msoko ya bidhaa ilipitishwa na Bunge mwaka 2015 na kanuni za soko la bidhaa ziliztolewana Waziri wa Fedha mwaka 2016, mchakato wa kukamilisha sakafu ya bishara ulianza mwaka 2017 na soko la biashara Tanzania lilianza rasmi mwaka 2018,’ amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Jackton Manyerere amewashauri TMX kutumia vyombo vya habari ipasavyo kuelezea kazi wanazofanya kwa kina ili wananchi waelewe zaidi fursa zinazopatikana ndani ya soko hilo la bidhaa Tanzania.

“Kwa muda mrefu TMX mmekuwa kimya lakini kuna mengi mazuri mnayafanya hivyo shirikianeni na vyombo vya habari katika kutangaza fursa zilizopo ndani ya TMX na wananchi wanufaike,” amesema Manyerere.

By Jamhuri