Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, ameachiliwa huru siku chache kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo uliopangwa kufanyika Machi 24.

Bwana Sonko na msaidizi wake Bassirou Diomaye Faye, walikuwa katika gereza la Cap Manuel na kulakiwa na maelefu ya watu.
.
Wakili wa Sonko Bamba Cisse, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba, mteja wake aliyekuwa anazuiliwa gerezani pamoja na mshirika wake mkubwa Bassirou Diomaye Faye wameachiliwa huru.
.
Faye tayari ameteuliwa kuwa mgombea wa upinzani baada ya Sonko kuzuiwa kuwania nafasi hiyo na haikujulikana mara moja namna hatua hiyo inavyoweza kuwa na athari kwenye uchaguzi huo.