Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani limechagua Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu kuwa Raisi wa Mkutano wa 153 wa umojahuo unaoendelea jijini Arusha.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu akisalimiana na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Uingereza (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle wakati wa Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) leo Oktoba 6, 2026. Zungu aliambatana na Wawakilishi wa Bunge la Tanzania IPU.