Na Mwamvua Mwinyi,JamhuriMedia,Pwani

Matumizi ya taa za kuongoza magari katika Makutano ya barabara eneo la KwaMathias yameanza tangu Septemba 07 usiku .

Aidha ,kwasasa mpango huo ,kazi inaendelea katika Makutano ya Mlandizi.

Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Pwani inaendelea na utekelezaji wa mpango kazi wa kupunguza msongamano katika barabara ya TANZAM.

Meneja wa TANROADS mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage amesema katika Mpango huo taa za kuongoza magari zitawekwa katika Makutano ya KwaMathias, Kwa Mfipa na Mlandizi.

Aidha, ameeleza kwamba ukarabati wa Barabara ya zamani ya Morogoro na njia za mchepuko(Diversions) zitaimarishwa na kuwekewa alama za barabarani.

Mwambage amebainisha kwamba mpango wa kudumu ni Utekelezaji wa mradi wa Kibaha-Chalinze-Morogoro Expressway (Km 205) kwa utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi(Public Private Partnership,P3) na Utekelezaji wa Mradi huo upo katika hatua za manunuzi.

By Jamhuri