
Historia ya vyama vya ukombozi yaibuliwa Windhoek
Leo ni Mei Mosi, Siku ya Wafanyakazi Duniani. Siwezi kukwepa taratibu za itifaki kwa kutoa salamu za pongezi kwa wafanyakazi wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu kwetu sote leo. Salamu maalumu napenda kuzitoa kwa wanahistoria kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutafiti na kuandika historia yetu kwa manufaa ya vizazi vyote, vya sasa na vya baadaye….