TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imefanya  tathmini ya miradi 1,800 na kati ya miradi hiyo 171 yenye thamani ya Sh bilioni 143.3 ilibainika kuwa na utekelezaji hafifu na hivyo kuanzisha uchunguzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru,  Salum Hamduni ameitaja  miradi hiyo ilikuwa katika sekta ya ujenzi, fedha, maji , kilimo pamoja na majengo

“Mapendekezo 3,668 yalitolewa ili kubainsha na kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika miradi hiyo, tumependekeza  marekebisho yafanywe ama kwa  gharama za mkandarasi au fedha iliyofujwa irudishwe serikalini,”amesema Hamduni

Pia amesema Takururu imezuia mali zinazodhaniwa kupatikana kutokana na rushwa ambayo ni magari 15 mashamba sita, hoteli tatu, nyumba za kulala wageni nne, viwanja 29,  nyumba za makazi 25 baa mbili, fremu mbili za maduka na shule moja ya sekondari.

By Jamhuri