Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma
KAMISHNA wa Uhifadhi ,Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA ) William Mwakilema amesema mtu yeyote anayetaka mnyama aitwe kwa jina lake atatakiwa kulipia gharama ya kiasi cha shilingi mil.5 ,lakini pia anayetaka kumuasili mnyama atatakiwa kulipia mil.1 kila mwaka kwa ajili ya kumuhudumia.

Akizungumza leo Julai 24,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa TANAPA kuhusu uhifadhi na kukuza utalii kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Kamishna huyo amesema kuwa hali itasaidia kuchochea ari ya kutangaza Utalii duniani.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa shirika linatarajia kuwezesha shughuli mbalimbali kwa gharama ya bil.118.3 pamoja na shilingi bil.60.6 kutekeleza miradi ya maendeleo.

Amesema kuwa kiwango cha makusanyo hayo yanayotarajiwa ni sawa na ongezeko la kiasi cha bil.56.3 sawa na asilimia 19 ukilinganisha na kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 ikionesha kuendelea kukua kimapato ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa hapo awali kabla ya UVICO 19 kuivamia dunia ambayo ilifanya mapato kupungua kwa kiwango kikubwa.

“Katika kipindi hicho cha mwaka 2018/2019 shirika liliweza kufikia makusanyo ya mapato kiasi cha bil.282.5”amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa shirika limejipanga kuendelea kuboresha miundombinu ya utalii kama barabara za utalii,viwanja vya ndege na malazi ili kuvutia watalii na kuongeza mapato,ili kuweza kupokea ongezeko la wageni kutokana na juhudi za Rais Dk,Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vilivyoko nchini kupitia filamu ya Tanzania “The Royal Tour”.

Akizungumzia uwekezaji na fursa zilizopo Kamishna huyo amesema kuwa TANAPA itawahamashisha wawekezaji wenye huduma za malezi katika hifadhi kuangalia uwezekano wa kutoa huduma nafuu kwa watalii wa ndani.

By Jamhuri