Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amelikabidhi Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tuzo ya mshindi wa pili kati ya Mashirika ya Umma ya Huduma na Biashara 306, kwa Utendaji Bora katika Usimamizi wa Fedha (Best Financial Management Performance – Commercial Entities).
Tuzo hiyo imetolewa Septemba 30, 2026, jijini Arusha, katika kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum), ambapo TANESCO imetambuliwa kwa utendaji bora katika usimamizi wa fedha na rasilimali za Shirika.
Tuzo hiyo imepokelewa na Bw. Plasduce Mbossa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, ikiwa ni heshima na pongezi kwa jitihada zinazofanywa na Shirika katika kuhakikisha fedha na rasilimali zake zinasimamiwa kwa ufanisi.
Tuzo hiyo ni sehemu ya utambuzi wa taasisi za umma zinazofanya vizuri katika usimamizi wa fedha, ikiwemo udhibiti wa matumizi, ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa rasilimali na kuimarisha uwajibikaji wa kifedha.



