Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imehakikisha utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka; barabara ya Nyerere hadi Gongo la mboto unaendelea huku barabara ya kawaida ikiendelea kupitika hata katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali Nchini.

Akizungumza wakati alipofanya ziara katika mradi huo Meneja wa miradi ya mabasi yaendayo haraka (BRT-3) iliyopo chini ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Frank Mbilinyi amesema amefanya ukaguzi wa kawaida kumuimiza mkandarasi kuhakikisha pamoja na athari za mvua lakini barabara inapitika wakati wote.

“Tumeendelea kumuhimiza mkandarasi kuhakikisha maeneo yote yanayotekelezwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyerere – Gongolamboto yanapitika kiurahisi pamoja na athari za mvua kila baada ya mvua kukatika ahakikishe anaziba mashimo na kusawazisha ili kuwezesha kurejesha mawasiliano ya barabara japo kuna ujenzi unaendelea” Amesisitiza na kuongeza kuwa

“Tunashirikiana vizuri na mkandarasi kuhakikisha anapokea maelekezo pale anapokuwa amerudi nyuma tunakumbusha pamoja mhandisi elekezi ili kuhakikisha kazi inafanyika vyema”

Aidha amewasa madereva wa magari kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za uendeshaji barabarani ili kuondoa changamoto wakati huu wa mvua kubwa.

By Jamhuri