Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma.

Serikaki kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS)imesaini Mikataba saba ya ujenzi wa barabara itakayo tekelezwa kwa miaka minne yenye thamani ya shilingi Trillion 3.7 yenye urefu wa kilometa 2035 kwa kiwango cha lami.

Mikataba hiyo imehusisha Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea Arusha – Kibaya – Kongwa Construction Of Handeni – Kiberashi – Kijingu – Njoro – Olboroti Mrijo Chini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida Igawa .

Nyingine ni Songwe – Tunduma Masasi – Nachingwea – Liwale Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River – Lalago – Maswa Construction Of Mafinga – Mtwango – Mgololo ambapo kila mkandarasi anayehusika na mradi mkubwa, atakua na timu nne za ujenzi katika kutekeleza Mradi.

Akizungumza leo June 16,2023 Jijini hapa kwenye hafla hiyo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ameeleza kuwa Barabara hizo zitajengwa Kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F).

Ameeleza kuwa utaratibu huo utaendelezwa katika miradi mingine mipya inayotekelezwa kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kwamba hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kuwa Makandarasi wa miradi yote saba (7) wamepatikana na kueleza kuwa mara mradi huo utakapo kamilika utasaidia kufungua fursa za kiuchumi katika maeneo zinapopita na kwa Taifa kwa ujumla.

Prof.Mbarawa ameeleza kuwa barabara zitakazojengwa zitapita katika Mikoa kumi na 13 na kufafanua kuwa Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo.

Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa yenye (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa; Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki.

“Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma; Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale,”amesema

Kwa upande wa Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa yenye (km 339), Waziri huyo amesema inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa huku barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga Mjini.

Aidha amefafanua kuwa katika Mradi wa Barabara ya Igawa – Tunduma (km 218) ambao utajengwa kwa njia nne (4), imepangwa barabara hiyo ifanyiwe usanifu na ujenzi utakaowezesha kuifanya njia moja kuwa ya malori tu, na yatatumia njia hiyo kwa kulipia pia, itajengwa barabara ya mchepuo (ByPass) ambayo itapita Nje ya Jiji la Mbeya.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta ameuzungumzia mradi huo kuwa wa kwanza kufanyika hapa nchini kutokana na ukubwa wake na kueleza kuwa mchakato wa zabuni za EPC+F ulifanyika kupitia ushindani wa uwazi ulioanza tarehe 27 Juni, 2022 ambapo jumla ya Makandarasi 129 walionesha nia.

Amesema Mchakato wa zabuni ulipitia hatua mbalimbali na hatimaye baada ya uchambuzi, ilibainika kwamba Makandarasi wanne (4) walikidhi vigezo vilivyowekwa ambao tutasaini nao mikataba leo. Makandasi hao ni:

Mhandisi Besta amewataja makandarasi hao kuwa ni Kampuni ya China Civil Engineering Construction (CCECC) ikishirikiana na kampuni ya China Railway 19th Bureau Group Corporation Ltd (CR19) kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd. kampuni ya China Overseas Engineering Group Co, Ltd (COVEC) pamoja na kampuni ya China Railway No. 4 Engineering Group Co. Ltd (CREC4)na Kampuni ya China Railway 15th Bureau Group (CR15G).

“Makandarasi hawa wote kupitia utaratibu wa EPC+F, watawajibika kufanya usanifu wa kina (Design) na kujenga barabara hizi kwa viwango na ubora ulioainishwa kwenye Mikataba na Vihatarishi vyote (risk) vinavyohusu usanifu wa mradi na muda wa ujenzi vitabebwa na Mkandarasi,”amefafanua.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa utaratibu huo utawezesha Makandarasi kusanifu na kujenga barabara kwa Viwango na teknolojia za kisasa na kwamba Wakala huo utasimamia ujenzi wa barabara hizo kwa mujibu wa vigezo na masharti yaliyopo kwenye mikataba na kwamba Makandarasi watakua na timu nne (4) kwa kila mradi mkubwa ili kuharakisha utekelezaji wa Miradi hiyo.

Please follow and like us:
Pin Share