Rais Samia Suluhu Hassan amezindua matokeo ya Sensa ya Watu na Mkazi kwa mwaka 2022 ambapo amesema kuwa Tanzania ina watu milioni 61, 741, 120.

Akizindua matokeo ya Sensa leo Oktoba 31,2022 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wastaafu, amesema kuwa sensa iliyofanyika imetimiza vigezo vya kimataifa hivyo Tanzania ina idadi ya watu 61, 741, 120.

Kati ya idadi hiyo 59,851,357 wapo Tanzania bara na watu 1,889,773 wako Tanzania Zanzibar.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 44,928,923 hii inaonesha kumekuwepo na ongezeko la watu 16,812,197 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 kati ya ongezeko la mwaka 2012 na mwaka 2022.

”Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, ya mwaka 2022, kuhusu matokeo ya Idadi ya watu duniani ya mwaka 2012, dunia ilikuwa na watu bilioni 7 na ilitarajiwa kuongezeka hadi kufikia bilioni nane mwaka huu 2022, hili ni ongezeko la watu bilioni moja katika kipindi cha miaka 10” amesema Rais Samia.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa mwaka 2022 bara la Afrika hususani katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara lina jumla ya watu bilioni 1.2 idadi inayokadiriwa kuongezeka hadi kufikia watu bilioni 2.1 ifikapo mwaka 2050

Amesema kuwa sensa iliyofanyika Agosti mwaka huu ilitimiza vigezo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na matokeo yake yanaweza kutumika kitaifa na kimataifa.

Rais Samia amesema kuwa sensa ya mwaka huu ni ya kihistoria kwani pia ilifanyika sensa ya anwani za makazi na sensa ya majengo ambapo tangu ilipofanyika mwaka 1961 .

Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa na linalofanyika kila baaada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwishi kufanyika ile ya mwaka 2012.

Sensa iliyofanyika ya mwaka 2022 ilikuwa ni sita ya sita kufanyiika nchini baada ya ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 19964.Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967,1978,2002 na 2012.

By Jamhuri