Na Mwandishi Wetu, JAMHURI MEDIA Lusaka Zambia

Tanzania na Zambia zimeingia makubaliano katika maeneo mnne ya ushirikiano na mikataba mnne ya miradi mbalimbali.

Mikataba hiyo na hati za makubaliano zimesainiwa mbele ya Rais Samia na Rais Hichilema wa Zambia katika Ikulu ya taifa Hilo Leo Oktoba 25,2023.

Jumla ya hati hizo nne za makubaliano na ushirikiano ni pamoja na

Hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Wakala wa Maendeleo Zambia

Hati ya Makubaliano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Wakala wa Maendeleo Zambia

Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zambia katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu

Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu programu ya kubadilishana Wakufunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu.

aidha kwa upande wa Mikataba jumla ya ya Mikataba mnne imesainiwa ikiwemo.

Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu programu ya kubadilishana Wanafunzi wa Kozi ya Afisa-Cadet.

Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu ushirikiano katika Huduma za Tiba.